Mto Salawin (kwa Kiingereza: Salween) ni mto mkubwa katika Asia ya Kusini-Mashariki. Chanzo chake kipo Tibet (China) halafu unapita Myanmar na Uthai kwenye mwendo wake wa takriban kilomita 2,400[1].

Mto Salawin
Chanzo Barafuto kwenye Nyanda za Juu za Tibet
Mdomo Bahari ya Andamani
Urefu km 2,815
Kimo cha chanzo m 5,350
Mkondo m3 4,978
Eneo la beseni km2 324,000

Majina yake hutofautiana kadiri ya nchi ambako unapita: Watibet huuita Nag Qu, pale China huitwa 怒江 Nù Jiāng, pale Myanmar Thanlwin Myit (pamoja na majina mengine) na mwishoni katika Uthai Maenam Salawin (แม่น้ำสาละวิน).

Mto huo unatokea kwenye Nyanda za Juu za Tibet na kuelekea magharibi mwanzoni. Lakini baadaye unageuka mashariki na kusini ukiishia katika Bahari ya Andamani huko Mawlamyaing, Myanmar.

Kwa njia ya kilomita 120 hivi mto huu ni mpaka baina ya Uthai na Myanmar, sehemu yake ya mwisho kabla ya bahari unarudi tena ndani ya Myanmar.

Marejeo hariri

  1. Salween Basin, Year: 2011, Water Report 37, tovuti ya Aquastat ya FAO

Marejeo mengine hariri

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Salawin kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.