Mto Zhu Jiang
22°46′N 113°38′E / 22.767°N 113.633°E
Chanzo | (vyanzo tofauti) |
Mdomo | Bahari ya Kusini ya China |
Nchi | China |
Urefu | km 2,400 |
Kimo cha chanzo | m |
Tawimito upande wa kulia | Xi Jiang na Bei Jiang |
Tawimito upande wa kushoto | Dong Jiang |
Mkondo | m3 9,500 |
Eneo la beseni | km2 453,700 |
Miji mikubwa kando lake | Guangzhou, Dongguan, Shenzhen, Zhongshan, Zhuhai, Macau, Hongkong |
Mto Zhu Jiang (kwa Kiingereza: Pearl River, "mto wa Lulu", zamani ilijulikana pia kama Canton River) ni jina la delta kubwa ya mito mbalimbali inayoishia kwenye Bahari ya China Kusini, na pia jina la pamoja kwa mfumo wa mito inayoungana hapa. Mito hiyo hujulikana kama mito ya Xi ("Magharibi"), Bei ("Kaskazini"), na Dong ("Mashariki") katika jimbo la Guangdong.
Kuanzia chanzo cha mto Xi, mfumo wote wa Zhu Jiang huwa na urefu wa km 2,400. Kwa hiyo ni mto mrefu wa tatu wa China baada ya Mto Yangtze na Mto Njano. Kufuatana na mkondo wa maji unayobeba ni mto mkubwa wa pili baada ya Yangtze. Jumla ya beseni lake ni km2 409,480. Beseni hilo linapokea pia maji kutoka kaskazini mwa Vietnam.
Mdomo wa mto Zhu Jiang ni kama hori ya bahari. Kabla yake liko jiji la Guangzhou. Hori ya mwisho inatenganisha Macau na Zhuhai upande wa magharibi na Hong Kong pamoja na Shenzhen upande wa mashariki.
Tawimito
hariri- Bei (北江)
- Dong (东江)
- Xi (西江)
- Yu (鬱江)
- Yong (邕江)
- Zuo (左江)
- You (右江)
- Yong (邕江)
- Xun (浔江)
- Qiang (黔江)
- Liu (柳江)
- Rong(融江)
- Hongshui (红水河)
- Beipan (北盘江)
- Nanpan (南盘江)
- Ba (灞水 or 灞河)
- Gui (桂江)
- Li (漓江)
- Yu (鬱江)
Picha
hariri-
Mto na Mnara wa Kanton
-
Mto wa Pearl usiku, Guangzhou
-
Daraja la Humen, likitazamwa kutoka Zhenyuan
-
Visiwa vya Zhuhai na Jiuzhou, vinatazamwa kutoka Kisiwa cha Yeli kwenye mdomo wa Mto wa Pearl
Marejeo
haririMakala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Zhu Jiang kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |