Mto Njano
Mto Njano (kwa Kichina: Huang He) ni mto mkubwa wa China ya Kaskazini, mto mkubwa wa pili wa China yote na mto mrefu wa nane duniani. Jina limetokana na rangi ya matope ya ardhi unamopita.
Mwendo wake una urefu wa kilomita mnamo 5,000 (viwango mbalimbali hutajwa kati ya kilomita 4,845 hadi 5,464) kuanzia nyanda za juu za Tibet hadi delta yake kwenye Bahari ya Bohai ambayo ni sehemu ya Bahari ya Mashariki ya China.
Kabla ya kufika baharini, mto unapita katika Tambarare ya China Kaskazini ambako ustaarabu wa China ulianzishwa. Ndiyo sababu Mto Njano umeitwa mara nyingi mto mama wa China na chanzo cha ustaarabu wa Kichina.
Rutuba ya ardhi ya tambarare hiyo ilijengwa na Mto Njano kwa kusambaza matope kwa miaka milioni kadhaa wakati wa mafuriko yake ya kimajira.
Viungo vya Nje
- Yellow River Home Page at UMassD Archived 1 Desemba 2005 at the Wayback Machine.
- Yellow River delta Information at LSU
- Listen to the Yellow River Ballade from the Yellow River Cantata
- "A Troubled River Mirrors China’s Path to Modernity" New York Times November 19, 2006
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Njano kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |