Adya juma
Ushiriki wa kiraia ni kitendo kinachohusisha mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu katika kushughulikia mambo yanayohusu jamii. Ushiriki wa kiraia unahusisha jamii zinazofanya kazi kwapamoja au mtu mmoja mmoja anaefanya shughuli za kisiasa na zisizo za kisiasa kwa lengo la kulinda maadili ya umma au kuleta mabadiliko katika jamii. Lengo la ushiriki wa kiraia ni kuwasilisha matakwa ya jamii na kulinda usawa katika jamii.[1]
Ushiriki wa kiraia ni kitendo kinachohusisha watu kufanya kazi kwapamoja ili kulinda matakwa au mahitaji ya jamii, "kazi kwa ajili ya demokrasia " (Checkoway & Aldana, 2012). Chini ya uwakilishi wa vikundi vya watu wachache, watu wenye kipato cha chini na vikundi vya vijana. Kwa upande mwingine, masuala yenye vikundi vya watu wenye ushawishi mkubwa yanawasilishwa kwa haraka ili kutatua matatizo yanayoikumba jamii hiyo. (Griffin & Newman, 2008).
Faida na changamoto
haririUshiriki wa kiraia kwa ujumla unakuza ushirikishwaji wa jamii na serikali kutokana na (ICMA: Leaders at the Core of Better Communities.). Umuhimu wa ushiriki wa kiraia ni kama ifuatavyo.
• Kufikia maamuzi yasiyo nje na sheria.
• Inajenga uaminifu kati ya wananchi na serikali ambayo inasaidia kujenga tabia katika mikutano ya hadhara.
• Kufikia malengo yenye matokeo chanya kwenye masuala magumu pia inasaidia viongozi waliochaguliwa na wananchi kutatua matatizo mbalimbali.
• Inakuza mawazo na kupata suluhu.
• Inatengeneza wananchi wanaojituma na kupunguza wahitaji katika jamii.
• Inafanya kazi kuwa rahisi.
Kwenye faida za ushiriki wa kiraia kuna changamoto zake. Changamoto zinatokana na sababu tofauti kutokana na (ICMA)kama ukosefu wa uaminifu, ufafanuzi wa majukumu na mda wa kuyafanya majukumu husika.
• Ushiriki wa kiraia unachukua mda kuonyesha mabadiliko chanya kuliko serikali ikifanya yenyewe moja kwa moja.
• Ushiriki wa kiraia ili ufanikiwe lazima kuwe na uwazi na uaminifu unahitajika kati wananchi na serikali.
Mchango wa jamii
haririUshirikiano wa jamii unahusisha nafasi za kidemokrasia ambapo watu wako tayari kujadili masuala mahususi kuhusu maslahi ya jamii na mbinu za kufanya mabadiliko yanayohitajika. Wananchi wanaweza kupata taarifa kuhusu mabadiliko yajayo, suluhu zinazopendekezwa kwa matatizo yaliyopo, n.k. Vyuo vikuu vinatoa fursa zaidi na kutarajia wanafunzi zaidi kushiriki katika kazi ya kujitolea katika jamii.
Teknolojia
haririMatumizi ya Televisheni
haririPutman aliangalia kwanini mtaji wa kijamii umekuwa ukipungua kwenye mojawapo ya maeneo ambayo utafiti huo ulifanywa na televisheni na kuona athari zake katika shughuli za kijamii na kiraia. Shah anaandika kwamba Putnam alipata kadiri televisheni mtu anavyotazama, ndivyo anavyokuwa hai katika shughuli za nje. Hii inaonyeshwa na kuongezeka kwa televisheni mnamo mwaka 1960 ushirikiano wa kiraia. Waligundua kwamba ingawa habari na programu za elimu zinaweza kusaidia maarifa ya kiraia, lakini ukosefu wa kujihusisha na shughuli za nje na matukio ya kijamii huumiza ushiriki.
Marejeo
hariri- ↑ "ushiriki wa kiraia". www.apa.org.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |