Muziki wa dansi wa kielektroniki

Muziki wa dansi wa kielektroniki (kutoka Kiingereza: "Electronic dance music"; kifupi: EDM; pia huitwa muziki wa klabu, au dansi[1]) ni muziki ambao huundwa kwa kutumia vifaa vya umeme.

Tamasha ya EDM katika mji wa Stockholm, nchi ya Uswidi.

EDM ni maarufu katika klabu, matamasha ya muziki, na sherehe za dansi ambazo huitwa raves. Unachezwa na MaDJ ambao wanachanganya nyimbo mbalimbali zenye midundo ya mtindo mmoja. EDM ina aina mbalimbali, kama house, tekno, transi, ngoma na besi, dubstep, trap, na nyingine nyingi.[2]

Kutoka mwanzoni mwa miaka ya 1980 hadi mwishoni mwa miaka ya 1990, EDM ilipata umashuhuri barani Ulaya. Wakati huohuo katika nchi ya Marekani, elektro na Chicago house—aina za EDM—zimekuwa maarafu kidogo. Sasa, EDM ni maarufu sana katika Ulaya, Marekani, na Australia; inakuwa maarufu zaidi katika Asia, Amerika ya Kusini, na Afrika pia. Music Trades—jarida la masuala ya muziki—lilisema katika mwaka 2013 kwamba umashuhuri wa EDM umeongezeka kwa kasi kuliko namna nyingine zote za muziki.[3]

Historia na aina za EDM hariri

Aina za muziki kama dub, hip hop, disko, na synth-pop ni aina za awali kabisa za muziki wa EDM. Aina za EDM katika miaka ya 1980 zilishusisha post-disko, elektro, house, tekno, na asidi house; katika miaka ya 1990 zilishirikisha transi, ngoma na besi, jungle, na breakbeat hardcore. Hizi aina zimebadilika na kuwa aina nyingi zaidi leo.

Dubstep hariri

Dubstep ilianza mjini London ya Kusini mwishoni mwa miaka ya 1990. Ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na mfumo wa sauti wa Jamaika.[4] Baadhi ya wasanii maarufu wa dubstep ni Skrillex, Bassnectar, na Excision.

House hariri

Muziki wa house ni aina kubwa zaidi ya EDM inayohusisha aina nyingine ndogondogo za muziki wa house, kama tekno house, deep house, future house, big room house, tropical house, na progressive house. Muziki wa house ulianzia mjini Chicago mwanzonu mwa miaka ya 1980. Muziki wa house hutumia sauti ya ala za mapigo nane-kwa-nane. Baadhi ya wasanii wamaarufu wa muziki wa house ni Carl Cox, Oliver Heldens, na Martin Garrix.

Trap hariri

Trap ni mchanganyiko wa hip hop, tekno, dub, na house ya Kiholanzi. Trap ilikuwa maarufu mwishoni mwa miaka ya 2000 na mwanzoni mwa miaka ya 2010. Baadhi ya wasanii maarufu wa trap ni RL Grime, Baauer, na Flosstradamus.

Mabishano hariri

Muziki huu wa dansi huhusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya, na huitwa madawa ya klabu kama MDMA, kokeini, ketamine, na madawa mengine. Katika baadhi ya matamasha ya muziki, watu wamekufa[5] baada ya kutumia madawa ya klabu.

EDM—kama aina nyingine za muziki kama roki—pia huhusishwa na mapenzi huria. Katika Uganda, Simon LokodoWaziri wa Nchi wa Maadili na Uaminifu—alijaribu kupiga marufuku tamasha la Nyege Nyege, tamasha kubwa la muziki mjini Jinja, kwa sababu alisema tamasha hilo linatangaza mapenzi huria na ushoga (hata hivyo hakuweza kulizuia tamasha Nyege Nyege).[6]

Wasanii wengine wamekosoa utamaduni wa EDM kwa sababu wanadhani sasa EDM imejikita katika biashara zaidi kuliko sanaa. Wasanii wengi wanalaumu utamaduni wa Marekani kwa kubadilisha EDM na kuifanya iwe na mrengo wa kibiashara.[7]

Marejeo hariri

  1. Koskoff (2004), p. 44; Koskoff, Ellen (2004). Music Cultures in the United States: an Introduction. Routledge. ISBN 9780415965897.
  2. "An Idiot's Guide to EDM GenresTrap". Complex (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-24. 
  3. "Music Trades November 2013 Page68". digitaleditions.sheridan.com (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-07-24. 
  4. Reynolds, S.(2012),Energy Flash: A Journey Through Rave Music and Dance Culture, Perseus Books; Reprint edition (5 Jan 2012), pages 511–516, (ISBN 978-1-59376-407-4).
  5. Kwai, Isabella (2018-09-17), "Are Music Festivals to Blame for Overdose Deaths?", The New York Times (kwa en-US), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2019-07-25 
  6. "Ugandan cabinet minister fails in bid to get Nyege Nyege Festival cancelled over LGBT 'celebration'". Resident Advisor. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-25. Iliwekwa mnamo 2019-07-25. 
  7. Fusilli, Jim (2012-06-06), "The Dumbing Down of Electronic Dance Music", Wall Street Journal (kwa en-US), ISSN 0099-9660, iliwekwa mnamo 2019-07-25 
  Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muziki wa dansi wa kielektroniki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.