Mzungu Kichaa
Mzungu Kichaa (pia anajulikana kama Espen Sørensen) ni mwimbaji na vilevile mwanamuziki kutoka nchini Denmark. Alizaliwa nchini Denmark, lakini kakulia nchini Tanzania, ambapo wazazi wake walikuwa wakifanya kazi katika masuala ya Maendeleo ya Ushirika. Walikwenda nchini Tanzania akiwa na umri wa miaka sita.
Mzungu Kichaa | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Espen Sørensen |
Pia anajulikana kama | Kichaa Espen |
Amezaliwa | Denmark |
Asili yake | Denmark |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Mwimbaji/Mwanamuziki |
Miaka ya kazi | 2001-hadi sasa |
Studio | Bongo Records |
Ame/Wameshirikiana na | Solo Thang Juma Nature Professor Jay |
Huko Tanzania amejifunza Kiswahili fasaha na baadaye kujihusisha na masuala ya muziki hasa katika utayarishaji wa muziki wa Bongo Flava katika studio ya Bongo Records. Matokeo ya hivi karibuni katika kujihusisha kwake na muziki huko Afrika ya Mashariki ni albamu yake ya kwanza ya kujitegemea iliyokwenda kwa jina la "Tuko Pamoja".
Shughuli za Muziki
haririMwishoni mwa miaka ya 1990 Espen Sørensen alikuwa miongoni mwa wasanii wa mwanzo kabisa kurekodi katika Studio ya Bongo Records huko mjini Dar Es Salaam. Wengineo walikuwepo kina Juma Nature, TID, Mangwair, Ferooz na Professor Jay. Wakati huo ilikuwa pia, ndipo alipopata jina lake la kisanii la Mzungu Kichaa.[1] Kwa bahati mbaya hakuonekana katika orodha ya wasanii chipukizi wa Tanzania kwa kipindi hicho, lakini pia alifanikiwa kufanya viitikio kadha wa kadha katika nyimbo kibao kwa kipindi cha mwaka wa 2001.[2]
Baadaye akaenda zake nchini Uingereza kusomea masuala ya Utamaduni wa Muziki na Anthropolojia. Baada ya kumaliza elimu ya masomo ya Kiafrika, akarudi tena katika shughuli zake za muziki, na kuanzisha kundi lililoitwa Effigong mnamo mwaka 2006. Mwaka wa 2008, akaamua kuwa msanii wa kujitegemea hadi kufanikiwa kutoa albamu yake ya kwanza kunako mwaka wa 2009 katika studio ya kujitegemea iliyoitwa Caravan Records.[3]
Albamu ilitolewa kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki, lakini baada ya kupata kupigwa sana katika baadhi ya vituo vya maredio kadhaa nchi za Ulaya, basi ikapelekea albamu pia kutolewa Ulaya mnamo mwezi Mei 2009. Baadhi ya nyimbo kutoka katika albamu ni pamoja na "Jitolee" (akiwa na Professor Jay) na "Wajanja" ambazo zote zimeimbwa kwa Kiswahilii, lugha ambayo inatumika sana katika Bongo Flava Afrika Mashariki.
Mashairi ya nyimbo zake yanalenga hasa matatizo ya kijamii huko nchini Tanzania, hasa umaskini.[4] Sørensen ametumia wiki tatu kufanya ziara ya kuitangaza albamu yake kuanzia mwezi wa Februari 2009, hasa nchini Tanzania na Kenya, lakini pia alipata kutumbuiza nchini Denmark akiwa na msaada wa kundi la ReCulture. Kibao cha Jitolee imepata kuwika sana nchini Tanzania na Kenya.[5]
Diskografia
hariri- Tuko Pamoja (2009)
- Hustle (2012)
- Relax (2014)
Marejeo
hariri- ↑ http://www.standardmedia.co.ke/archives/InsidePage.php?id=1144006484&cid=123 Mzungu Kichaa: Danish with love for African music
- ↑ Mzungu Kichaa
- ↑ Biography
- ↑ Mzungu Kichaa. Tuko Pamoja - Debut Album Ilihifadhiwa 30 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Daily Nation, 29 Januari 2010: Bongo star’s latest single a big hit
Viungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mzungu Kichaa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |