Nabii Azaria (jina la Kiebrania עֲזַרְיָה, ‘Ǎzaryā, lina maana ya "YHWH amesaidia"; alizaliwa karne ya 10 KK) alikuwa nabii wa Israeli ya Kale ambaye habari zake zinapatikana katika Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati sura ya 15.

Mfalme Asa akivunja sanamu kwa kuhimizwa na nabii Azaria.

Humo tunasoma kwamba, baada ya kushukiwa na Roho Mtakatifu, alikwenda kwa mfalme Asa wa Yuda kumhimiza afanye urekebisho wa kidini.

Kweli mfalme huyo alivunja sanamu za miungu na kujenga upya altare ya YHWH katika hekalu la Yerusalemu.

Baada ya hapo kulitokea kipindi cha amani kwa miaka 35.

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabii Azaria kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.