Nabii Nahumu (kwa Kiebrania נחום, yaani "Aliyefarijiwa na Mungu") alikuwa nabii mjini Yerusalemu katika karne ya 7 KK, wakati wa mfalme Yosia, aliyetawala Yuda kati ya mwaka 640 KK na 609 KK.

Nabii Nahumu katika picha ya Waorthodoksi ya karne XVIII.

Mahubiri yake yanatunzwa katika Kitabu cha Nahumu ambacho ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya gombo la Manabii wadogo katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na kwa hiyo pia katika Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kitarehe kinashika nafasi kati ya kile cha nabii Mika na kile cha Habakuki.

Kinashangilia kwa ufasaha wa kishairi ujio wa maangamizi ya dola la Waashuru na ya makao yao makuu, Ninawi (612 KK): hivyo maadui wa taifa na wa Mungu hatimaye wataadhibiwa.

Kwa jumla alitangaza kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayetawala nyakati zote na kuhukumu mataifa kwa haki[1].

Tangu kale Nahumu anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Desemba[2][3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabii Nahumu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.