Nassima Saifi (* 29 Oktoba 1988) ni mwanariadha mlemavu kutoka nchini Algeria. Anashindana hasa katika mchezo wa kurusha tufe na kurusha kisahani. Alipata medali ya dhahabu mbili katika fani zote mbili wakati wa michezo ya Paralimpiki akawa bingwa wa dunia mara tatu.

Maisha hariri

Saifi alizaliwa mjini Mila (Algeria) mwaka 1988.[1] Alizaliwa mzima lakini baada ya ajali akiwa na umri wa miaka 10 alipotewa na mguu wote wa kushoto.[2]

Baba yake alimtia moyo wa kuingia katika riadha. Alijiunga na klabu ya michezo ya Mila alipopata mazoezi na mafundisho. [3]

Kwa msaada wa baba yake Saifi alishiriki mara ya kwanza kwenye uwanja wa kimataifa aliposhiriki mashindano ya ubingwa wa dunia ya michezo ya walemavu mwaka 2006 huko Uholanzi akiingia kwa tiketi ya Algeria. Alifikia nafasi ya tano kwa kurusha tufe na pia nafasi ya tano kwa kurusha kisahani.

Saifi alifika kwenye michezo ya paralimpiki mwaka 2008 huko Beijing akishiriki kwa kurusha tufe na kisahani akimaliza nafasi ya kumi na ya nne.

Alifaulu mwaka 2011 kwenye mashindano ya ubingwa wa dunia ya michezo ya walemavu mjini Christchurch (New Zealand) ambapo alishiriki tena kwa kurusha tufe na kisahani. Hapo alishinda medali ya dhahabu kwa kufikia mita 40.99 kwa kisahani. [4]

Mwaka uliofuata akafika kwenye Michezo ya Paralimpiki ya 2012 huko London akapata medali za dhahabu kwa kurusha tufe na kisahani.

Mwaka 2013 kwenye mashindano ya Ubingwa wa Dunia huko Lyon alitetea cheo chake kwa kisahani lakini alifaulu pia kupata medali ya bronzi kwa kurusha tufe.

Miaka miwili baadaye mjini Doha Saifi alifaulu kutetea tena cheo chake cha bingwa wa dunia kwa kurusha kisahani.

Katika maandalizi kwa ajili ya Paralimpiki alifanya mazoezi masaa matatu kila siku akifundishwa na kocha Hocine Saadoun.

Saifi aliimarisha nafasi yake kati ya wanariadha bora wa paralimpiki wakati wa Michezo ya Paralimpiki ya 2016 huko Rio de Janeiro. Alipata tena medali ya dhahabu kwa kisahani na fedha kwa tufe.

Maelezo hariri

  1. "Saifi, Nassima". Paralympic.org. Iliwekwa mnamo 4 September 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Saifi, Nassima". IPC. Iliwekwa mnamo 4 September 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "Nassima Saifi, championne du monde du lancer de disque" (kwa French). DjaZairess. Iliwekwa mnamo 19 February 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)(French). DjaZairess. Iliwekwa mnamo 19 February 2017.
  4. "Rio Paralympics 2016 (Discus-women/T57): Gold medal for Algerian Nassima Saifi". aps.dz. 15 September 2016. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-27. Iliwekwa mnamo 26 October 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)