Nathari ni tawi mojawapo la fasihi andishi. Tofauti na tenzi au ushairi unaoleta ujumbe wake kwa umbo la mabeti, nathari haina umbo maalumu au viwango vya muundo au taratibu. Hivyo inaweza kufanana na mazungumzo ya kila siku.

Nathari inafaa kwa habari na masimulizi. Kwa mfano inatumiwa kwenye magazeti, vitabu, jarida au kamusi.

Ni tungo za kisanii za kubuni ambazo hutumia lugha ya kimaelezo mfululizo na kiinsha/mjazo kupasha ujumbe wa kuelimisha, kuburudisha.

Hujumuisha: riwaya, hadithi fupi, insha za kifasihi.

Marejeo hariri

  • Wamitila, K.W. 2003. Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus Books.
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nathari kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.