Neema ya utakaso ni istilahi inayotimiwa na Kanisa Katoliki kumaanisha neema muhimu kuliko zote ambazo mtu anaweza kupewa na Mwenyezi Mungu. Inatiwa na Roho Mtakatifu rohoni ili kuiondolea na dhambi na kuifanya takatifu.

Neema ya utakaso inatazamwa muhimu zaidi kwa sababu ni uzima wa Mungu unaotiwa ili mtu aweze kutenda kwa upendo wake na kujiandaa aishi naye milele. (Yoh 1:16; 3:3-8; Ef 3:4-7; 2Pet 1:3-4)

Kadiri ya imani hiyo, mtu hawezi kuhakikisha neema ya utakaso kwa kuwa ni tukio ambalo linapita maumbile na kufanyika rohoni, hivyo halifikiwi na hisi zetu. Pengine Mungu anatokeza dalili fulani za badiliko hilo kama vile furaha ya ndani au karama ya nje, lakini hizo hazihitajiki wala hazitoshi kuthibitishia mtu amepata neema hiyo. (Math 7:22-23; 1Kor 13:1-3)

Kwa kawaida mtu anapata neema ya utakaso mara ya kwanza katika Ubatizo. Uzima huo mpya unatarajiwa kustawi duniani na kudumu hata milele. (1Kor 3:1-3; Eb 5:11-14)

Mtu anapoteza neema ya utakaso kwa dhambi yoyote kubwa. (Lk 8:13-14; 11:24-26; Yoh 15:1-2; Rum 11:20-22; 1Kor 10:12; 2Pet 2:20-22)

Ikiwa Mkristo amepoteza neeema ya utakaso atarudishiwa kwa sakramenti ya Kitubio au hata kwa majuto kamili akiwa na nia ya kupokea sakramenti hiyo. (Lk 22:31-32; Rum 11:23,29; 1Yoh 2:1-2)

Marejeo

hariri
  • Pohle, J. (1909). Sanctifying Grace. In The Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. [1]
  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Neema ya utakaso kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.