Injili ya Luka ni kitabu cha tatu katika orodha ya vitabu vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Huhesabiwa kati ya Injili Ndugu pamoja na Injili ya Mathayo na Injili ya Marko.

Mlo wa Emau , mchoro huu wa Caravaggio (1601) unaonyesha habari mojawapo bora ya Injili ya Luka.
Agano Jipya

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Vitabu viwili, kazi moja

hariri

Injili ya tatu, ya Mtakatifu Luka, inaendelezwa na kitabu cha Matendo ya Mitume: katika dibaji za vitabu vyake hivyo mwandishi anaeleza sababu na taratibu za kazi yake kwa mlengwa wa kwanza, Teofilo. Mtu huyo hajulikani, na pengine jina hilo linawakilisha msomaji yeyote, hasa kwa sababu linatafsiriwa "Mpenzi wa Mungu".

Mwandishi

hariri

Kadiri ya mapokeo, mwandishi ni mganga Luka, mwenzi wa Mtume Paulo katika safari zake kadhaa.

Inawezekana kwamba alikuwa mwenyeji wa Antiokia (Syria); kwa vyovyote hakuwa Myahudi, yeye peye yake kati ya waandishi wote wa Biblia.

Muda na malengo

hariri

Wataalamu wanakisia kwamba aliandika vitabu vyake kwenye miaka 80-90, akitumia Injili ya Marko, kitabu cha misemo ya Yesu kinachotajwa kifupi kama Q na vyanzo vingine vya habari.

Katika Injili hiyo mambo yote yanalenga Yerusalemu, kiini cha jiografia ya wokovu, wakati katika Matendo ya Mitume yote yanaanzia huku na kulenga miisho ya dunia.

Inaonekana kuwa aliandika baada ya maangamizi ya Yerusalemu na ya hekalu lake mwaka 70, akitaka kuthibitisha uaminifu wa Mungu kwa ahadi zake, yaani kwamba matukio hayo ya kutisha yalisababishwa na Wayahudi kwa kumkataa Masiya wao, Yesu Kristo.

Kwa sababu hiyo, Mungu aliendeleza mpango wake wa wokovu kwa kuwalenga moja kwa moja mataifa yote.

Luka anasisitiza habari njema kwamba wokovu ni kwa wote, hasa wasiotarajiwa: maskini, wakosefu, wanawake n.k.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Tafsiri ya Kiswahili

hariri
  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili

Ufafanuzi

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Injili ya Luka kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.