Shoro (Acrocephalidae)

(Elekezwa kutoka Nesillas)
Shoro
Shoro mkuu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Acrocephalidae (Ndege walio na mnasaba na shoro)
Salvin, 1882
Ngazi za chini

Jenasi 7:

Shoro ni ndege wadogo wa familia Acrocephalidae. Spishi za familia Locustellidae (zamani Megaluridae) zinaitwa shoro pia. Ndege hawa wana rangi ya kahawa au kijivu mgongoni na nyeupe au njano chini. Spishi nyingi huhamia Afrika wakati wa majira baridi huko Ulaya. Spishi za Acrocephalus zinatokea mahali yenye matete, mafunjo au uoto mwingine wa maji katika Afrika, Asia na Ulaya; spishi nyingine hupenda miti au vichaka. Hula wadudu. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa majani na pengine vijiti. Tago la spishi za Acrocephalus limefungiwa mabua ya matete. Jike huyataga mayai 2-6.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri