Niseti wa Lyon (pia: Nicetius, Nicetus, Nicet au Nizier; 513 hivi - 2 Aprili 573) alikuwa askofu mkuu wa mji huo wa Gaul (leo Ufaransa) kwa miaka 20 baada ya ndugu ya mzazi wake Saserdosi wa Lyon aliyefariki mwaka 552[1].

Alijulikana kwa upendo wake kwa maskini na kwa uzinguaji wa pepo[2]. Pia aliratibu liturujia.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3] au tarehe 3 Desemba.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.