Njiwa habari (kwa Kiing. homing pigeon) ni aina maalum ya njiwa. Njiwa hao hufugwa kwa shabaha ya kuweza kurudi nyumbani kutoka mahali popote, hata kwa umbali mrefu sana, wakibeba habari. [1]

Njiwa habari
Njiwa habari akibeba ujumbe mguuni.

Misingi ya kibiolojia

hariri

Kati ya njiwa mwitu ndiye Njiwa-miamba mwenye uwezo huo wa kurudi kwenye kiota chake na kwa mwenza wake. [2]

Hadi leo hakuna uhakika kamili kuhusu uwezo huo. Wataalamu wanaona ndege hao wanahisi ugasumaku wa Dunia. Kuna pia dalili kwamba ndege kadhaa wanaweza kutambua nyota na hivyo kukadiria mwelekeo kwa umbali mkubwa[3].

Kwa hiyo ufugaji ulianza na njiwa-miamba. Njiwa za kufugwa walirekodiwa kuwa na uwezo wa kurudi kwa umbali wa kilomita 1,800. [4] Kasi hadi 95 km/h ilithibitishwa. [5]

Matumizi

hariri

Njiwa hao hutumiwa kubeba ujumbe na habari. Hapo habari inaandikwa kwenye kipande kidogo cha karatasi nyepesi kinachoviringishwa na kufungwa kwenye mguu wa njiwa.

Njiwa anaweza kurudi tu mahali anapokumbuka ni nyumbani kwake. Kwa hiyo anayetuma habari anahitaji kushika njiwa kutoka mahali anapotaka kutuma ujumbe na kusafiri naye.

Historia

hariri
 
Wanajeshi Waingereza wakimtuma njiwa habari mwaka 1945

Taarifa za kwanza kuhusu njiwa habari zimehifadhiwa kutoka Misri ya Kale. Zilitumiwa mara nyingi na wanajeshi waliotaka kufikisha ujumbe haraka.[6]

Tuna taarifa kwamba Wagiriki wa Kale walitumia njiwa kutangaza washindi wa Michezo ya Olimpiki. Njiwa habari walitumiwa pia katika mfumo wa posta wa makhalifa wa Baghdad[7]

Katika karne ya 19 njiwa habari walitumiwa katika huduma ya habari kama Reuters waliokuwa na njiwa 46 wa kubeba habari za soko la hisa baina ya Brussels na Aachen penye mwisho wa nyaya za telegrafu.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza na ya Pili njiwa habari walitumiwa sana na pande zote mbili. Jeshi la Uswisi lilikuwa na kitengo cha njiwa habari hadi mwaka 1996.[8]

Marejeo

hariri
  1. Levi, Wendell (1977). The Pigeon. Sumter, S.C.: Levi Publishing Co, Inc. uk. 82. ISBN 0853900132.
  2. Blechman, Andrew (2007). Pigeons-The fascinating saga of the world's most revered and reviled bird. St Lucia, Queensland: University of Queensland Press. ISBN 9780702236419. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-01-12. Iliwekwa mnamo 2009-12-23.
  3. https://www.scientificamerican.com/article/homing-pigeons-remember-routes-for-years/ Homing Pigeons Remember Routes for Years, Tovuti ya Scientific American, 1 Machi 2022
  4. Walcott, Charles (1996). "Pigeon Homing: Observations, Experiments and Confusions" (Pdf article). Journal of Experimental Biology. 199 (Pt 1): 21–27. doi:10.1242/jeb.199.1.21. PMID 9317262. Iliwekwa mnamo 2008-01-04.
  5. "The Speed of Birds". BBC.Co.UK. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (Web article) mnamo 2009-02-20. Iliwekwa mnamo 2008-01-04.
  6. https://www.jstor.org/stable/44563742 Carter W. Clarke: Signal Corps Pigeons , The Military Engineer, Vol. 25, No. 140 (MARCH-APRIL, 1933), pp. 133-138 (6 pages)
  7. "The Sport of Racing Homing Pigeons". fbipigeons.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-14. Iliwekwa mnamo 2003-09-17. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)
  8. https://www.admin.ch/cp/d/1996Jul17.170649.6345@idz.bfi.admin.ch.html Auflösung des Brieftaubendienstes abgeschlossen, tovuti ya serikali ya Uswisi , Julai 1996