Alfred Nobel

(Elekezwa kutoka Nobel)

Alfred Nobel (21 Oktoba 183310 Desemba 1896) alikuwa mhandisi na mwenye viwanda wa nchi ya Sweden.

Alfred Nobel

Mwaka wa 1867 aligundua jinsi ya kutengeneza baruti kali. Pia aliboresha utoneshaji wa mafuta. Akafaulu kiuchumi akawa tajiri na wakati uleule mwenye wasiwasi kuhusu matumizi ya baruti aliyogundua kwa sababu aliona matumizi mabaya kwa ajili ya silaha. Hivyo katika hati yake ya wasia alianzisha Tuzo ya Nobel kwa ajili ya mafanikio ya kisayansi lakini pia kwa ajili ya amani duniani.

Kuanzia ilipoanzishwa tuzo ya Nobel watu mbalimbali wametunukiwa tuzo hiyo kama vile Albert Einstein, Niels Bohr, Max Planck, Mama Teresa, Nelson Mandela n.k.


Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alfred Nobel kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.