Nyanda za Juu za Mongolia

Nyanda za Juu za Mongolia ni sehemu za Nyanda za Juu za Asia ya Kati zinazoenea katika Mongolia na kaskazini mwa China kwa takriban kilomita za mraba 3,200,000. Inapakana na Milima ya Hinggan Kubwa upande wa mashariki, Milima ya Yin upande wa kusini, milima ya Altai upande wa magharibi, na milima ya Sayan na Khentii upande wa kaskazini. [1]

Ndani ya nyanda za juu liko Jangwa la Gobi na pia maeneo makubwa ya nyika kavu. Mwinuko uko takriban mita 1,000 hadi 1,500 juu ya u.b.

Kisiasa, eneo lote limegawanywa kati ya Mongolia, China na Urusi. Upande wa China, sehemu za Mongolia ya Kichina na mkoa wa Xinjiang ni sehemu ya nyanda za juu za Mongolia. Huko Urusi, ni sehemu za Buryatia na kusini mwa Irkutsk Oblast.

Historia

hariri

Nyanda za juu hizo zilikaliwa na kuvamiwa na vikundi mbalimbali katika mwendo wa historia, pamoja na Xiongnu, Xianbei, Waturuki wa Gök, nasaba ya Tang, nasaba ya Liao, Milki ya Wamongolia, na nasaba ya Qing.

Mazingira yanayobadilika

hariri

Tabianchi inazidi kuwa yabisi. Maziwa mengi kwenye Nyanda za Juu za Mongolia kama vile Qagaan Nurr na Ziwa la XinKai, yamepungua kwa theluthi mbili za eneo lake la uso. Mengine yamekauka kabisa; Huangqihai na Naiman Xihu yamekauka kabisa kati ya miaka 1980 na 2010. Wakati maziwa machache kama vile Ziwa la Mashariki la Juyan na Had Paozi yamekoma, kwa wastani eneo lote la maziwa limepungua kwa 30%. [2] [3]

Marejeo

hariri
  1. Zhang, Xueyan; Hu, Yunfeng; Zhuang, Dafang; Qi, Yongqing; Ma, Xin (2009). "NDVI spatial pattern and its differentiation on the Mongolian Plateau". Journal of Geographical Sciences. 19 (4). Springer-Verlag: 405. doi:10.1007/s11442-009-0403-7.
  2. "Shrinking Lakes on the Mongolian Plateau". NASA. 8 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Tao, Shengli; Fang, Jingyun; Zhao, Xia; Zhao, Shuqing; Shen, Haihua; Hu, Huifeng; Tang, Zhiyao; Wang, Zhiheng; Guo, Qinghua (17 Februari 2015). "Rapid loss of lakes on the Mongolian Plateau". Proceedings of the National Academy of Sciences. 112 (7): 2281–2286. doi:10.1073/pnas.1411748112. PMC 4343146. PMID 25646423.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyanda za Juu za Mongolia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.