Nyanda za juu za Ngorongoro

Nyanda za juu za Ngorongoro (kwa Kiingereza: Ngorongoro Highlands au Crater Highlands) ni eneo lenye miinuko lililopo kwenye bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki katika mikoa ya Arusha na Manyara, kaskazini mwa Tanzania.

Ramani ya nyanda za juu za Ngorongoro, inatazamwa kutokea kaskazini kuelekea kusini.

Jiolojia

hariri

Nyanda za juu za Ngorongoro zinapatikana katika mgawanyiko ambapo bamba la Afrika linagusana na bamba la Somalia, kukutana kwa mabamba haya mawili husababisha maumbile mapya ya kijiolojia kujitokeza.[1]

Kama ilivyo kawaida, sehemu za mgawanyiko kati ya mabamba ya gandunia, maumbile ya kivolkeno huwepo. Hivyo nyanda hizo zina kasoko nyingi na kaldera za kivolkeno. Magma, hupanda kupitia nyufa zilizotokea na kufika kwenye uso wa ardhi na kuunda umbo la koni. Kaldera huundwa pindi volkeno ikilipuka au kuporomoka ndani yake.[1]

Jiografia

hariri

Yafuatayo hupatikana kwenye nyanda za juu za Ngorongoro:

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "Crater Highlands". NASA Earth Observatory. Iliwekwa mnamo 29 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)