Ospisi wa Nizza (alifariki Cap Ferrat, Villefranche-sur-Mer, leo kusini mwa Ufaransa, 580 hivi) alikuwa Mkristo wa Misri aliyeishi miaka mingi kama mkaapweke katika mnara wa zamani karibu na Nizza, na ndipo alipofariki.

Sanamu yake.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Mei[1][2].

Maisha hariri

Gregori wa Tours alisema watu mbalimbali waliwahi kuandika juu ya Ospisi, lakini habari zilizotufikia ni zile tu alizoziandika mwenyewe[3], akimsifu kwa juhudi zake na kwa karama zake za unabii na miujiza. Kati ya mengine, alitabiri uvamizi wa Walombardi[4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.