Otilia wa Alsasya

(Elekezwa kutoka Otilia wa Hohenbourg)

Otilia wa Alsasya, O.S.B. (pia Odilia wa Alsace; 662 hivi - Mont Sainte-Odile, 720 hivi) alikuwa mwanamke wa ukoo maarufu wa Alsace (leo nchini Ufaransa).

Mt. Otilia huko Avolsheim, Alsace

Inasemekana alikataliwa na baba yake kwa sababu ya jinsia yake na ya upofu wake, hivyo alilelewa na wakulima.[1]

Miujiza mbalimbali ilitokea katika maisha yake baada ya kupata ubatizo na kuwezeshwa kuona.

Hapo kwa msaada wa baba yake, alianzisha monasteri mbili za Kibenedikto na kuwa abesi wake hadi alipofariki dunia[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Mwaka 1807 Papa Pius VII alithibitisha heshima hiyo.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Desemba[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "Saint Odilia of Alsace". Saints.SQPN.com. Iliwekwa mnamo 2012-07-14.
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/81200
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Sala kwa Mt. Otilia, msimamizi wa macho

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.