Oxfam
Oxfam International ni kikundi cha mashirika 14 yanayofanya kazi na zaidi ya wabia 3,000 katika nchi karibu 100. Shabaha yake ni kupata suluhisho la kudumu la umaskini na udhalimu. [1]
Oxfam inaelimisha umma kuhusu shida hizo, huendesha miradi ya kuleta mabadiliko, na hutoa msaada katika majanga makubwa, pia inakuza maendeleo endelevu na biashara ya haki (fair trade).
Oxfam ilianza mjini Oxford, Uingereza, mnamo 1942 kama Kamati ya Oxford ya kupambana na Njaa, kwa hiyo imechukua jina kutoka maneno Oxford na "Famine". Ilianzishwa na wafuasi wa Jamii ya Marafiki (Quaker), wanaharakati wa kijamii, na wasomi wa Oxford. [2]
Hii sasa ni Oxfam Great Britain, ofisi yake bado iko Oxford, Uingereza. Shabaha yao ya kwanza ilikuwa kushawishi serikali ya Uingereza kufikisha chakula kwa watu wa Ugiriki iliyovamiwa na Ujerumani na Italia wakati ya Vita Kuu ya Pili. Baada ya vita shirika iliendelea kutafuta chakula kwa watu katika nchi za Ulaya zilizoharibika vitani, pamoja nchi za maadui kama Ujerumani.
Kazi ya Oxfam ilianza kupanuka wakati wa kuundwa kwa shirika la Oxfam nchini Kanada mnamo 1963.
Marejeo
hariri- ↑ Statement from the Oxfam website.
- ↑ Cecil Jackson-Cole from Oxfordshire Blue Plaques Board. Ilihifadhiwa 11 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine. Retrieved 22 October 2009.