Paolo Maldini
Paolo Maldini, (alizaliwa tarehe 26 Juni 1968) alikuwa mchezaji gwiji wa AC Milan na timu ya taifa ya Italia akicheza kama beki wa kushoto na pia beki wa kati alicheza misimu 25 akiwa na AC Milan kabla ya kustaafu akiwa na umri wa miaka 41 mwaka 2009.
Alishinda mataji 23 akiwa na Milan: UEFA Champions League mara tano, mataji ya Serie A mara saba, Coppa Italia mara moja, Supercoppa Italiana mara tatu, European Super Cups mara nne, Intercontinental Cups mara mbili na FIFA Club World Cup mara moja.
Maldini alianza kuichezea Italia mwaka 1988 akiichezea kwa miaka 14 ambayo ni rekodi iliyovunjwa na Fabio Cannavaro mwaka 2009 na Gianluigi Buffon mwaka 2013. Maldini alikuwa nahodha wa Italia kwa miaka 8 na kuvaa kitambaa cha unahodha mara 74 mpaka alipomuachia Cannavaro 2010. Akiwa na Italia, Maldini alishiriki kwenye michuano ya UEFA European Championship mara tatu na FIFA World Cups mara nne.Ingawa hakushinda taji lolote akiwa na Italia, alifikisha Italia kwenye fainali za 1994 Kombe la dunia na Euro mwaka 2000,na nusu fainali za Kombe la dunia mwaka 1990 na Euro 1998. Alichaguliwa pamoja na timu yao iliyong'ara kwenye michuano ile pamoja na Euro 1996.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Paolo Maldini kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |