Parisi, O.S.B. Cam. (Bologna, Italia, 1160Treviso, 11 Juni 1267) alikuwa mmonaki padri tangu umri wa miaka 12 hadi alipofariki anayo 108[1].

Kati ya miaka hiyo yote, aliitumia 77 iliyofuata upadrisho wake (1191) katika kuongoza kiroho monasteri ya masista wa shirika lake pamoja na kuhudumia wageni na wagonjwa walioifikia monasteri hiyo[2].

Kutokana na miujiza mingi iliyotokea kwa maombezi yake akiwa hai na baada ya kifo chake, askofu wa Treviso, Alberto Ricco, alimtangaza mtakatifu tarehe 25 Novemba 1268[3].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Juni[4][5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.