Pepe Kallé (30 Novemba 1951 - 28 Novemba 1998) alikuwa mwimbaji wa soukous, mwanamuziki na kiongozi wa bendi kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Pepe Kallé alipozaliwa alipewa jina Kabasele Yampanya katika mji mkuu wa Kinshasa (wakati huo mji huu ulikuwa unajulikana kama Léopoldville), lakini baadaye aliamua kulichukua jina la mshauri wake, Grand Pepe Kalle.

Pepe Kalle mnamon mwaka 1978
Pepe Kallé
Jina la kuzaliwaKabasele Yampanya
Amezaliwa(1951-11-30)30 Novemba 1951
Léopoldville, Kongo ya Kibegiji
Amekufa28 Novemba 1998 (umri 46)
Miaka ya kazi1960-1998

Muziki na maisha

hariri

Pepe Kalle alikuwa na uwezo wa kuimba kwa sauti ya juu zaidi pamoja na sauti ya chini zaidi ambayo kwa lugha ya kimombo inaitwa “multi-Octave range”. Pepe Kalle alikuwa akiingia jukwani anatambulika mara moja kwani alikuwa na urefu wa sentimita 190 (fiti 6 inchi 3) na uzito wa kilogramu 136 (puandi 300). Mwimbaji huyu alirekodi zaidi ya nyimbo mia tatu na Albamu ishirini katika wasifu wake wa miongo miwili mirefu ya muziki. Kwa wapenzi wake wa muziki alikuwa anajulikana kama "tembo wa muziki Halisi ya Afrika " na "La Bombe Atomique" kwani Pepe Kalle aliwatumbuiza watazamaji tendaji zake za nguvu.

Wasifu wake wa kimuziki ulianza na African Jazz, bendi ya Grand Pepe Kalle. Baadaye akawa mwimbaji kiongozi wa Lipua Lipua, ambapo aliimba sambamba na Nyboma Mwandido. Mwaka wa 1972, Pepe Kalle pamoja na Dilu Dilumona na Papy Tex, waliiacha bendi ya Lipua Lipua na kuunda bendi yao wenyewe iliyokuwa ikiitwa Empire Bakuba. Empire Bakuba ilichukua jina lake kutoka kabila ya kishujaa ya Kikongo, na kundi hili lilingiza ngoma na midundo ya muziki kutoka ndanindani, sauti ambazo zilikuwa zimetupiliwa mbali kwa muda mrefu na rumba maarufu. Bendi hii ilikuwa maarufu mara moja na pamoja na Zaiko Langa Langa wakawa bendi za vijana maarufu zaidi katika mji mkuu wa Kinshasa. Pamoja na vibao motomoto kama Dadou ya Pepe Kallé na Sango ya mawa ya Papy Tex, bendi hii daima ilishirikishwa kwenye chati ya muziki. Wao pia waliumba njia mpya ya kucheza au kusakata iliyojulikana kama kwassa kwassa.

Katika mwaka wao wa kumi tangu kuanzishwa kwao mwaka wa 1982, bendi hii iliteuliwa kama kundi cha juu zaidi nchini Zaire. Katika miaka ya mapema ya 1980, Empire Bakuba iliendelea ziara zake za mbali huku ikitoa zaidi ya albamu nne kwa mwaka. Katikati ya miaka za 1980, walikuwa na wafuasi wengi katika Kati ya Francophone na Afrika Magharibi. Ushirikiano wake wa mwaka wa 1986 pamoja na Nyboma iliyokuwa ikiitwa Zouke Zouke ilikuwa mmoja kati ya Albamu zilizouzwa sana mwaka huo. Lakini ilikuwa ushirikiano wake wa pili na Nyboma, Moyibi (mwaka wa 1988), ambayo ilianzisha umaarufu wake kote Afrika.

Mwishoni mwa miaka ya 1980 na mapema miaka ya 1990, Pepe Kalle aliunganisha vipengele vya soukous vilivyochezwa kwa kasi ambavyo viliundwa katika studio za Paris. Albamu yake ya mwaka wa 1990, Roger Milla, iliyotoa shukrani kwa talanta na ujuzi wa mwanakandanda huyu mkuu kutoka Kamerun, ni mfano maridadi wa mpangilio huu.

Mwaka wa 1992, bendi ilikabiliwa na msiba wake wa kwanza mkubwa wakati Emoro, mbilikimo wa kusakata rhumba wa bendi, aliupa dunia mkono wa buriani wakati walikuwa ziarani nchini Botswana. Licha ya msiba huu, umaarufu wa Pepe Kallé uliendelea kuenea katika miaka ya tisini kwani alitoa Albamu kama Gigantafrique , Larger than life na Cocktail . Alishirikiana na wanamuziki wa kitambo mashuhuri kama vilevile Lutumba Simaro na Nyoka Longo.

Pepe Kallé aliaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo mnamo Novemba 1998.

Diskografia

hariri
Na. Jina la albamu Mwaka Maelezo
1 Et L'Empire Bakuba ‎– Untitled 1982 Albamu ya kwanza akiwa na Empire Bakuba, lakini ilikosa jina.
2 Bitoto 1985 Zaire
3 Soucis Ya Likinga 1986 Albamu ya kwanza kufanya akiwa nchini Ufaransa
4 Kwasa Kwasa 1987 Ya pili kutoka Ufaransa
5 Moyibi 1988 Ameshirikiana na Nyboma
6 L'Argent Ne Fait Pas Le Bonheur! 1988 Albamu ya pili ndani ya mwaka mmoja.
7 Pepe-Kalle 1989 Albamu yenye jina lake.
8 Pon Moun Paka Bougé 1989 Utaratibu wa albamu zaidi ya moja ndani ya mwaka mmoja inaendelea. Alifanya hivi mwaka 1988.
9 Atinze Mwana Popi 1989 Albamu ya tatu ndani ya mwaka mmoja.
10 Chante Le Poète Simaro Massiya 1989 Albamu ya nne ndani ya mwaka mmoja.
11 Gigantafrique! 1990
12 Le Tube De Vos Vacances : Liya Liya Faina 1990 Albamu ya pili ndani ya mwaka mmoja
13 Gerant 1991 Albamu ina wimbo wa maarufu Afrika Mashariki - hasa Tanzania "Shikamo Seye" au maarufu kama "Hidaya" wangu.
14 Divisé Par Deux 1992
15 Maya 1992 Albamu ya pili kutoka ndani ya mwaka mmoja na vilevile ya pili kufanya na msanii mwingine mbali na Empire Bakuba baada ya ile aliofanya na Nyboma 1988. Albamu ameshirikiana na "Lutumba Simaro".
16 Hommage À Emoro 1992 Albamu ya tatu kutoa ndani ya mwaka, ya pili kufanya na Nyboma tangu "Moyibi". Ya kwanza kufanya na "Bopol Mansiamina".
17 isanga Ya "Banganga" 1992 Albamu ya nne kutoa ndani ya mwaka mmoja, ya kwanza kufanya na marehemu "Tabu Ley".
18 Larger Than Life 1992 Albamu ya tano kutoka ndani ya mwaka mmoja. Albamu ina nyimbo kadhaa kutoka katika albamu zilizopita.
19 Mamie Music Clarification 1992 Albamu ya sita kutoa ndani ya mwaka mmoja, ya kwanza kufanya na Papy Tex
20 Sacrée Doudou 1992 Albamu ya saba kutoka ndani ya mwaka mmoja. Albamu ya kwanza kushirikiana na mwanamama "Doudou Bastide".
21 Gardez Votre Souffle 1993
22 Dieu Seul Sait 1997
23 Cocktail 1998 Na huu ndio mwaka aliokufa.
24 Pépé Kallé ? Mwaka haujulikani. Lakini ilisambazwa na "Mélodie Distribution" ya nchi Ufaransa
25 Milla ? Albamu haijulikani imetoka mwaka gani wala lebo ya usambazaji haijulikani. Lakini ina nyimbo za zamani ambazo zinatoka katika albamu zilizopita.
26 Pepe Kalle (albamu) 1990 Albamu ya pili yenye jina lake.
27 Album Lumière ?

Kompilesheni albamu

hariri

Hizi ni orodha ya albamu zilizotolewa kama kompilesheni au nyimbo mchanganyiko kutoka kwa Pepe Kalle.

Jina la albamu Mwaka
Zabolo 1997
Best Of Pepe Kalle 1998
The Best Of Pépé Kallé 1999[1]

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri