Petro, Dorotheo na Gorgoni
Petro, Dorotheo na Gorgoni (walifariki Nikomedia, leo Izmit nchini Uturuki, 303) walikuwa Wakristo waliofanya kazi katika ikulu wa kaisari Dioklesyano katika mji huo.
Kwa agizo la kaisari mwenyewe, Petro, aliyelalamikia mauaji ya kikatili ya Migdoni na wenzake, aliangikwa mtini hadharani na kuteswa muda mrefu sana kwa mijeledi; hatimaye alibanikwa akiwa hai. Wenzake Dorotheo na Gorgoni, kwa kulalamikia uuaji wake walipewa adhabu za namna hiyohiyo na hatimaye kunyongwa[2].
Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Jacobi a Voragine (cur. Th. Graesse), Legenda aurea (Lipsia, 1850), p. 601.
- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/44690
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |