Pharos ya Aleksandria


Pharos ya Aleksandria ilikuwa mnara wa taa mjini Aleksandria ya Misri ikahesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia. Kimo chake hakikujulikana kikamilifu lakini kilikuwa kati ya mita 110 na 150.

Pica ya Pharos kwenye sarafu za Aleskandria zilizotolewa wakati wa Dola la Roma.

Mnara huu ulijengwa kwenye kisiwa kidogo kilichoitwa "Pharos" kiliochokuwa mita chache mbele ya mwambao wa Aleksandria. Baadaye mnara uliitwa kwa jina la kisiwa.

Ujenzi ulitokea mnamo mwaka 282 KK. Kwa karne nyingi Pharos ilikuwa kati ya majengo marefu ya dunia. Iliporomoka baada ya matetemeko ya ardhi yaliyotokea Aleksandria 1303 na 1323.