Potamoni wa Herakleopoli

Potamoni wa Heracleopoli Magna (alifariki 341 au 345) alikuwa askofu wa mji huo wa wilaya ya Arkadia, nchini Misri.

Aliteseka kwa ajili ya imani ya Kikristo wakati wa dhuluma ya kaisari Masimino Daia (311); huyo, baada ya kumnyofoa jicho na kumlemaza mguu, alimpeleka kufanya kazi ya shokoa migodini.

Kisha kuachiliwa alishiriki mtaguso wa kwanza wa Nisea. Rafiki mwaminifu wa Atanasi Mkuu, alimtetea kwa ushujaa katika mtaguso wa Tiro (335) na kwa ajili hiyo alisaini pia barua ya wenzake kwa mwakilishi wa kaisari, Flavio Dionisi. Kwa sababu hiyo alichukiwa na Waario, waliofanya afukuzwe na kaisari Kostanzo kutoka jimboni mwake ili wamweke askofu mmoja wa kwao. Aliteswa kiasi cha kufa mwaka 341 au 345.

Anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe mbalimbali, hasa 18 Mei kwa kumchanganya na Potamoni mwingine aliyekuwa padri tu.

Tazama pia

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.