Prisko, Malko na Aleksanda

Prisko, Malko na Aleksanda (walifariki Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli, 257/258) walikuwa Wakristo ambao walifia imani yao. Walikuwa wanaishi shambani karibu na mji huo, walipouawa Wakristo wengi; basi, wakisukumwa na ari ya Kimungu, walijitokeza kwa hiari mbele ya hakimu kumlaumu kwa kuadhibu kikatili wacha Mungu tu, si wengine. Mara walitupwa kama chakula kwa wanyamapori wakati wa dhuluma ya Kaisari Valerian [1].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Machi[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.