Domobeleshi
(Elekezwa kutoka Prosymna)
Domobeleshi | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Domobeleshi wa Sundevall (Prosymna sundevalli)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 16:
|
Domobeleshi ni nyoka wasio na sumu wa jenasi Prosymna katika familia Lamprophiidae. Wamepewa jina hili kwa sababu hutumia domo lao kwa kuchimba kama beleshi.
Nyoka hawa ni wafupi, sm 45 kwa kipeo lakini sm 25-35 kwa kawaida. Rangi yao ni kijivu au kahawia mara nyingi pamoja na vidoa vyeusi au kijivubuluu. Spishi nyingine zina mabaka na nyingine zina rangi kali.
Domobeleshi huchimba katika udongo au mchanga mtifu ambapo hutafuta mayai ya mijusi na nyoka wengine. Hawaonekani sana isipokuwa wakati wa mvua.
Nyoka hawa hawana sumu kwa sababu hula mayai ya reptilia wengine tu. Kwa hivyo wanaweza kukamatwa bila shida. Lakini wakitishwa spishi kadhaa hujipinda katika zongomo na wakiguswa huzongoa na kuzonga tena upesi.
Spishi
hariri- Prosymna ambigua, Domobeleshi wa Afrika ya Kati (Central African shovel-snout)
- Prosymna angolensis, Domobeleshi wa Angola (Angolan snovel-snout)
- Prosymna bivittata, Domobeleshi Milia-miwili (Two-striped shovel-snout)
- Prosymna frontalis, Domobeleshi Kusi-magharibi (South-western African shovel-snout)
- Prosymna greigerti, Domobeleshi wa Greigert (Greigert's shovel-snout)
- Prosymna janii, Domobeleshi wa Msumbiji (Mozambique shovel-snout)
- Prosymna lineata, Domobeleshi Tumbo-jeupe (Lined shovel-snout)
- Prosymna meleagris, Domobeleshi Vidoadoa (Speckled shovel-snout)
- Prosymna ornatissima, Domobeleshi wa Uluguru (Ornate shovel-snout)
- Prosymna pitmani, Domobeleshi wa Pitman (Pitman's shovel-snout)
- Prosymna ruspolii, Domobeleshi wa Ruspoli (Ruspoli's shovel-snout)
- Prosymna semifasciata, Domobeleshi Mistari (Banded shovel-snout)
- Prosymna somalica, Domobeleshi Somali (Northern Somali shovel-snout)
- Prosymna stuhlmanni, Domobeleshi Mashariki (East African shovel-snout)
- Prosymna sundevalli, Domobeleshi wa Sundevall (Sundevall's shovel-snout)
- Prosymna visseri, Domobeleshi wa Visser (Visser's shovel-snout)
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Domobeleshi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |