Kidukari-sufu

(Elekezwa kutoka Pseudococcidae)
Kidukari-sufu
Kidukari-sufu wa “Solanum” (Phenacoccus solani)
Kidukari-sufu wa “Solanum” (Phenacoccus solani)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Linnaeus, 1758
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Lang, 1888
Oda ya juu: Paraneoptera
Oda: Hemiptera
Haeckel, 1896
Nusuoda: Sternorrhyncha
Familia ya juu: Coccoidea
Handlirsch, 1903
Familia: Pseudococcidae
Heymons, 1915
Ngazi za chini

Jenasi ±275

Vidukari-sufu au vidung'ata ni wadudu wadogo wa familia Pseudococcidae katika oda Hemiptera ya nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Licha ya jina lao wadudu hawa siyo vidukari kwa ukweli lakini aina za wadudu-gamba. Wanachoza nta kama wadudu-gamba wote lakini nta hii haiumbi aina ya gamba. Nta ina umbo wa nyuzi nyeupe ambayo zinawapa wadudu hawa jina lao.

Vidukari-sufu ni sumbufu kama wadudu-gamba wengine. Kinyume na jamaa wao wanasambaza virusi kwa sababu hutembea zaidi, k.m. virusi ya chipukizi lililofura ya mkakao (CSSV), virusi ya mnanasi ulionyauka na virusi ya majani yaliyosokotwa ya mzabibu (GRLaV). Hata shida ya kuvu inayokua kwa mana zao ni kubwa zaidi (angalia ukurasa wa kidukari). Adui wa vidukari-sufu ni sawa na wale wa wadudu-gamba: wadudu-kibibi, wadudu mabawa-vena na nyigu wa kidusia na pia kuvu viuawadudu (entomopathogenic fungi) kama Beauveria bassiana, Lecanicillium lecanii na Neozygites fumosa.

Vidukari-sufu ni wadogo. Kiwiliwili chao kimerefuka kidogo na kina urefu wa mm 2-5. Majike huchoza nyuzi za nta nyeupe zilizo na kifano cha sufu au unga (asili ya jina la Kiingereza mealybug). Majike hawana mabawa lakini wana miguu kinyume na wadudu-gamba wengine. Kwa kweli majike huhifadhi umbo wa lava ambayo huitwa neotenia (neoteny). Madume wana mabawa kwa sababu wanayahitaji ili kutafuta majike, lakini wana jozi moja tu, ile ya mbele. Mabawa ya nyuma yamepungua, mara nyingi mpaka alama tu. Madume wengi wanafanana na usubi au nzi wadogo.

Majike wa vidukari-sufu hutaga mayai au huatamia mayai katika ovarioli zao. Kinyume na wadudu-gamba lava wa kila hatua wa vidukari-sufu wana miguu. Kila mara wanapoambua huwa wakubwa zaidi mpaka kuwa wapevu. Wale wa kiume hupitia muda wa pumziko ambapo wanakuza mabawa (kama bundo lakini siyo kweli). Madume hawali na hufa baada ya kukwea majike kadiri ilivyowezekana.

Spishi zilizochaguliwa

hariri