Mpera
(Psidium guajava)
Mpera
Mpera
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Myrtales (Mimea kama mkarafuu)
Familia: Myrtaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mkarafuu)
Jenasi: Psidium
Spishi: P. guajava L., 1753

Mpera (Psidium guajava) ni mti mdogo wa familia Myrtaceae.

Matunda yake huitwa mapera. Asili yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini, lakini siku hizi unapandwa mahali pengi pa kanda za tropiki na nusutropiki.

Mti wa mpera unatoa dawa ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo kifua, tezi dume, nguvu za kiume, fizi, chunusi, n.k. Kwa ajili hiyo hatua ya kwanza unachukua majani ya mpera, unayasaga na kuyakausha, halafu weka maji na yachemshe majani ya mpera yaani kama chai. Baadaye chukua chupa ili uhifadhi tayari kwa matumizi. Pia majani ya mpera yanaponesha kisukari na kutibu wanawake walio na hedhi.

  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mpera kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.