Mfalme Radama I (kuzaliwa 1792 - kufariki 1828) alirithi kiti cha ufalme cha Andrianampoinimerina katika kisiwa cha Madagaska mwaka 1810 akiwa na umri wa miaka 18.

Radama I, mfalme 1810-1828.

Jukumu lake la kwanza kabisa baada ya kushika ufalme wa Merina lilikuwa kuyapiga makundi ya ndani ya ufalme huo yaliyoasi.

Hata hivyo, mafanikio yake makubwa zaidi yalihusiana na upanuaji wa mipaka. Alitafuta njia moja kwa moja hadi baharini ili kufanikisha biashara baina yake na Wazungu na kuupanua utawala wa Merina.

Jeshi lake si tu kuwa lilitumika kuyapiga majimbo mengine, bali pia kudumisha sheria na utulivu katika maeneo yaliyotekwa.

Hadi mwaka 1825, Radama alikwisha kuliteka eneo lote la pwani ya mashariki ya Bukini, kuanzia Vohema hadi ngome ya Dauphin. Aidha aliishinda sehemu kubwa ya magharibi, ila ilikuwa vigumu kuiteka Sakalava.

Pamoja na hayo yote, hadi mwaka 1823 Radama aliweza kuupanua utawala wa Merina katika sehemu kubwa sana ya kisiwa hicho.

Ingawa utawala wake katika kisiwa hicho chote haukukamilika, hakukuwa na kipingamizi chochote kikubwa dhidi ya kujitangaza kwake kuwa mfalme wa Bukini.

Alifariki mwaka 1828 akiwa na umri wa miaka 36.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Radama I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.