Raineri wa Split, O.S.B.Cam. (pia: Raynerius, Raniero, Ranieri, Renier, Rayner, Arnir; Italia, 1110 hivi - Split, leo nchini Korasya, 1180) alikuwa mmonaki wa urekebisho wa Wabenedikto wa Camaldoli.

Alikuwa askofu wa Cagli, Italia ya Kati miaka 1156-1175, halafu wa Split. Katika miji yote miwili alipigania haki za Kanisa na kwa ajili hiyo alisumbuliwa sana hata akauawa kwa kupigwa mawe[1][2].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini. Papa Aleksanda VIII alithibitisha heshima hiyo mwaka 1690.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 4 Agosti[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Catholic Encyclopedia (1913) : "Cagli e Pergola"
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/65460
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri
  • Acta Sanctorum, I, Antverpiae, 1643, pp. 354–357.
  • D. Farlati, Illiricum sacrum, III, Venetiis, 1765, pp. 194–210.
  • G. Palazzini, S. Rainerio (1100?-1180) arcivescovo e martire, Urbania 1945.
  • A. M. Zimmermann, Kalendarium Benedictinum, II, Wien, 1939, p. 560.
  • Novak, Grga, Povijest Splita I., Čakavski sabor, Split, 1978.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.