Rasi Delgado

(Elekezwa kutoka Rasi ya Delgado)

Rasi Delgado (kwa Kireno: Cabo Delgado) ni rasi mwambaoni mwa Bahari Hindi iliyoko kaskazini kabisa mwa pwani ya Msumbiji.

Rasi Delgado katika Msumbiji

Rasi Delgado iko takriban km 40 kusini kwa mji wa Mtwara, Tanzania. Mji mdogo wa Quionga umo rasini.

Historia

hariri

Baada ya kufukuzwa kwa Wareno kwenye pwani za Kenya na Tanzania ya leo, wakati wa karne ya 17, Rasi Delgado ilikuwa mpaka wa kaskazini wa maeneo yaliyobaki chini ya athira ya Ureno katika Afrika ya Mashariki.

Lakini katika karne ya 18 na 19, mamlaka ya Ureno haikutosha tena na kwenye Hori ya Tungi, upande wa kusini wa rasi, utawala wa Sultani wa Tungi ulijitegemea. Kuanzia mwaka 1858 Usultani wa Zanzibar ulieneza mamlaka yake hadi huko.

Baada ya kuenea kwa Wajerumani kwenye pwani ya Uswahilini, nguvu ya Zanzibar ilififia na Wareno waliweza kujenga utawala. Lakini mwaka 1894 Wajerumani walivamia maeneo upande wa kusini mwa Mto Rovuma ambayo baadaye yalikuwa na Pembetatu ya Kionga. Ureno ilipaswa kukubali utawala wa Kijerumani.

Katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Ureno ilitwaa pembetatu hiyo, na sasa mto Rovuma umekuwa mpaka wa Msumbiji hadi mdomo wake.

  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rasi Delgado kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.