Pembetatu ya Kionga
Pembetatu ya Kionga ilikuwa eneo dogo la kilomita za mraba 395 [1] kwenye Bahari ya Hindi, kusini kwa Mto Rovuma na kaskazini mwa Rasi Delgado. Ndani ya eneo hilo kuna mji wa Kionga (kwa Kireno "Quionga"), ambao mwaka wa 1910 ulikuwa na wakazi karibu 4,000.
Eneo hilo lilikuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani lakini tangu mwaka 1918 ni sehemu ya Msumbiji.
Historia
haririHistoria ya awali
haririMnamo karne ya 19 eneo karibu na Rasi Delgado lilitawaliwa na Usultani wa Tungi [2], ilhali Ureno ilidai pwani yote hadi Rasi Delgado, lakini haikuwa tena na mamlaka yoyote kaskazini mwa kisiwa cha Ibo. [3] Sultani wake aliishi kwenye Hori ya Tungi, kusini mwa rasi hiyo. Mwaka 1844 mtawala wa Zanzibar Said bin Sultani alikuwa ametangaza kwa Waingereza kwamba himaya yake ilienea hadi Rasi Delgado; lakini mwaka 1848 kutokana na udhaifu wa Ureno alimteua Sultani wa Tungi kuwa gavana, na mwaka 1854 Zanzibar ilimpeleka gavana wake pamoja na kikosi kidogo cha askari kwenda Tungi. [4]
Baada ya kuanzishwa kwa Afrika Mashariki ya Kijerumani mwaka 1885, nguvu ya Zanzibar ilififia. Wakati tume ya kuangalia mipaka ya Ujerumani-Uingereza-Ufaransa iliposafiri ufukweni mwaka 1886 ili kujua ukubwa wa eneo la Wazanzibari, gavana wa Ureno alituma msafara wa kijeshi katika sehemu ya kusini ya Hori ya Tungi, ambapo tume iliamua kuwa eneo la Zanzibar linaenea kusini hadi kwenye mdomo wa Mto Minengani [5] kwenye hori hiyo. [6] . Makubaliano yafuatayo ya mipaka baina YA Uingereza na Ujerumani ya tarehe 29 Oktoba 1886 yalirudia azimio hili, lakini yalitaja eneo la kutenganisha maslahi ya Uingereza na Ujerumani kuwa liliaNza tu kwenye Mto Rovuma. [7]
Kwenye Februari 1887 Wareno walivuka mto Minengani na kuvamia Tungi yenyewe; askari wa Sultani walijiondoa kwenye pwani wakikaa ndani. Serikali ya Sayyid Bargash wa Zanzibar ilipambana wakati uleule na madai ya Waingereza na Wajerumani kuwaachia sehemu za Kizanzibari za pwani za Kenya na Tanganyika za baadaye, hivyo haikuchukua hatua zozote kuwaondoa tena Wareno katika Tungi. Hivyo Wareno waliweza kuimarisha utawala wao hadi Rasi Delgado[8].
Mzozo wa Ureno na Ujerumani
haririKatika makubaliano yafuatayo ya Kijerumani-Kireno ya Desemba 30, 1886, mstari wa Rovuma kutoka mdomoni ulitajwa kuwa mpaka kati ya milki za Wareno na Wajerumani. [9] Ukanda wa pwani bado ulikuwa wa Zanzibar.
Katika Mkataba wa Helgoland-Zanzibar wa mwaka 1890, Ujerumani ilichukua eneo la kusini mwa ukanda wa bara wa Zanzibar katika pwani ya Afrika Mashariki, ingawa maandishi ya mkataba huo yalitaja tu "mpaka wa kaskazini wa jimbo la Msumbiji" na "njia ya mto Rovuma" kama mpaka wa kusini. Kwa hiyo, hali ya eneo la Kizanzibari upande wa kusini mwa Rovuma haikuwa wazi kimkataba.
Upande wa Ujerumani uliamua baadaye kidogo kuchukua udhibiti wa pande zote mbili za mdomo wa mto Rovuma na kumaliza mahali pa Kionga kama bandari ya magendo. [10] Kikosi cha wanamaji cha Ujerumani kilivamia eneo hilo tarehe 16 Juni 1894 na kuanzisha kituo cha Kionga penye ofisi ya forodha. [11] Hatimaye Ureno ilikubali kushiriki katika tume ya pamoja ya mpaka, ambayo mwaka wa 1895 ilikubali mpaka ambao ulipita kaskazini kidogo mwa Rasi Delgado kando ya latitudo 10° 40' hadi Rovuma, ambayo ilifuata kutoka hapa [12]. Hii ilianzisha "pembetatu ya Kionga".
Pembetatu ya Kionga katika Vita ya Kwanza ya Dunia
haririWakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia, Wareno walivamia eneo hadi Mto Rovuma mnamo 1916. [13] Dola la Ujerumani liliwahi kutangaza vita dhidi ya Ureno tarehe 9 Machi 1916. [14]
Tarehe 25 Septemba 1919 katika Mkataba wa Versailles Rovuma hatimaye ilifafanuliwa kama mto wa mpaka hadi mdomoni. Ureno ilipewa pembetatu ya Kionga kama fidia kwa uharibifu wa vita. Azimio kuhusu eneo la Tanganyika lilitambua mto Rovuma kutoka mdomoni hadi kuingia kwa mto Messinge ("M'Sinje") kuwa ni mpaka wa Msumbiji[15].
Pembetatu ya Kionga ilijumuishwa rasmi katika Afrika ya Mashariki ya Kireno kwa sheria n.º 962 tarehe 2 Aprili 1920.
Mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na udhamini wa Umoja wa Mataifa baadaye ulimalizika tarehe 25 Juni 1975 wakati wa uhuru wa Msumbiji, ambayo eneo hilo likawa sehemu ya jimbo la Cabo Delgado. [16]
Stempu za posta
haririTarehe 29 Mei 1916 Wareno walitoa stempu za posta za Kionga. Stempu za posta za zamani kutoka koloni la Lourenço Marques (leo Maputo) zilizo na picha ya Mfalme Carlos I na muhuri wa "REPUBLICA" (ufalme wa Ureno ulipinduliwa mwaka wa 1910) zilitumiwa. Kwa kuongeza, neno "Kionga" na thamani mpya ilichapishwa juu yake. Stempu zilithaminiwa kuwa ½, 1, na 2 ½ na 5 centavo. Stemu hizo zinachukuliwa kuwa adimu.
Kujisomea
hariri- H. B. Thomas: The Kionga Triangle. Tanganyika Notes and Records, Bd. 31, 1951, S. 47–50.
Viungo vya nje
hariri- Kionga Ilihifadhiwa 4 Machi 2016 kwenye Wayback Machine., Deutsches Koloniallexikon, Vol. 2, p. 303, Leipzig 1920.
Marejeo
hariri- ↑ Encyclopaedia Britannica: Quionga
- ↑ in älteren Texten auch "Tunghi"
- ↑ Norman R. Bennet: Zanzibar, Portugal, and Mozambique: relations from the late eighteenth century to 1890, Boston University African Studies Center ASC Working Papers in African Studies Series, S. 1+3, https://hdl.handle.net/2144/41078
- ↑ Bennett, S.7
- ↑ auch "Mnangani River"; heute: Rio Nambulala
- ↑ No. 2B1 — PROCES-VERBAL, containing the unanimous opinions of the Delegates of Great Britain, France, and Germany, with reference to the Maritime, Littoral, and Continental Possessions of the Sultan of Zanzibar. Zanzibar, 9th June, 1886; in: The Map of Africa by Treaty, ed. E. Hertslet, Vol. III. Part II., Nos. 260 to 373. Great Britain and Germany to United States, online https://archive.org/details/mapofafricabytre03hert/page/n5
- ↑ No. 264.—-AGREEMENT between the British and German Governments, respecting the Sultanat of Zanzibar and the opposite East African Mainland, and their Spheres of Influence. 29th October— lrst November, 1886. Map of Africa by Treaty S. 883
- ↑ Bennett uk. 16 ff
- ↑ 26. Erklärung zwischen der Kaiserlich Deutschen und Königlich portugiesischen Regierung, betreffend die Abgrenzung ihrer beiderseitigen Besitzungen und Interessensphären in Südafrika. Vom 30 . Dezember 1886. "Artikel 2. Die Grenzlinie, welche in Südostafrika die deutschen Besitzungen von den portugiesischen Besitzungen scheiden soll, folgt dem Laufe des Flusses Rovnma vou seiner Mündung bis zu dem Punkte, wo der Messinjefluß in den Rovuma mündet, und läuft von dort nach Westen weiter auf dem Breitenparallel bis zu dem Ufer des Nyassa -Sees."; in: Die Deutsche Kolonialgesetzgebung : Sammlung der auf die deutschen Schutzgebiete bezüglichen Gesetze, Verordnungen, Erlasse und internationalen Vereinbarungen mit Anmerkungen und Sachregister / auf Grund amtlicher Quellen hrsg. von Gerstmeyer, Dr. Köbner, Zweiter Theil 1893 bis 1897. Auf Grund amtlicher Quellen und zum dienstlichen Gebrauch herausgegeben von Dr. Alfred Zimmerman Berlin 1898, online https://brema.suub.uni-bremen.de/download/pdf/2157012?name=
- ↑ "Ohne Name: Der deutsch-portugiesische Grenzstreit, in: Karl Homann (Hrsg.): Neueste Mittheilungen. Berlin, 31. Juli 1894". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-03-16. Iliwekwa mnamo 2021-11-27.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help) - ↑ Nach Angaben im Großen Deutschen Kolonialatlas, herausgegeben von der Kolonialabteilung des Auswärtigen Amtes, bearbeitet von Paul Sprigade und Max Moisel, Berlin 1901–1915.
- ↑ 124. Abgrenzung der deutschen und portugiesischen Gebiete in Ostafrika. (Kol.-Bl . 1894, S . 486. Kol.-Bl . 1897, S . 194 ), in: Die Deutsche Kolonialgesetzgebung a.a.O., S. 135; online https://brema.suub.uni-bremen.de/download/pdf/2157012?name=
- ↑ Karte der deutschen und portugiesischen Militäroperationen am Kionga-Dreieck, engl.
- ↑ O Portal da História: A REOCUPAÇÃO DE QUIONGA, abgerufen am 3. August 2014.
- ↑ League of Nations Document C.449.1(a).M.345(Ca).1922.VI, ; Official Journal. III (1922), pp. 865-68; Terms of League of Nations Mandates, Republished by tbe United Nations, October, 1946, No. 9 , online hapa, uk. 303
- ↑ Lochner: Kampf im Rufiji-Delta. Wilhelm Heyne, München 1987, S. 424, ISBN 3-453-02420-6.