Kikucha (Regulus)

Ndege wadogo wa jenasi Regulus, familia Regulidae
(Elekezwa kutoka Regulidae)
Kikucha
Kikucha utosi-dhahabu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: incertae sedi (hali isiyo na hakika)
Familia: Regulidae (Ndege walio na mnasaba na vikucha)
Jenasi: Regulus
Cuvier, 1800
Ngazi za chini

Spishi 7:

Vikucha ni ndege wadogo sana wa jenasi Regulus, jenasi pekee ya familia Regulidae. Spishi za jenasi Sylvietta zinaitwa vikucha pia. Vikucha wa Regulus ni kijanikijivu wenye utosi njano au mwekundu. Katika Afrika wanatokea kutoka Maroko mpaka Tunisia na kisiwa cha Tenerife ndani ya misitu ya misonobari. Wanatokea pia Ulaya, Asia na Amerika ya Kaskazini. Hula wadudu ambao huwakamata juu mitini. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe kwa vigoga na kuvumwani lililoning'iniza mwishoni kwa tawi la juu la msonobari. Jike huyataga mayai 7-12.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri

Spishi ya kabla ya historia

hariri
  • Regulus bulgaricus (Mwisho wa Pliocene, Varshets, Bulgaria)