Rio Negro (Amazon)

(Elekezwa kutoka Rio Negro (Amazonas))

Rio Negro ni mto ambao unapitia msitu wa mvua wa Amazonas katika kaskazini-magharibi ya Brazil, kwenye jimbo la Amazonas.

Rio Negro
Rio Negro katika beseni ya Amazonas
Chanzo Nyanda za juu za Kolombia
Mdomo Mto Amazonas, karibu na mji wa Manaus
Nchi Kolombia, Venezuela, Brazil
Urefu km 2,250
Tawimito upande wa kulia Mto Vaupes
Tawimito upande wa kushoto Mto Branco
Mkondo wastani m3/s 28,400
Eneo la beseni km2 691,000
Miji mikubwa kando lake Manaus
Mto Rio Negro unapoishi kwenye mto Amazonas

Unaitwa Negro (Kihispania na Kireno kwa "nyeusi") kwa sababu maji yake yanabeba vyembe vya ardhi ambavyo hufanya maji yaonekane kama chai. [1] [2] Ni mto mkubwa wa maji meusi duniani.

Rio Negro ndiye tawimto kubwa zaidi la mto Amazonas upande wa kushoto (kadiri inavyoelekea bahari). Huanza huko Kolombia na kuishia kwenye Amazonas.

Rio Negro ina utajiri mkubwa wa spishi tofauti. Karibu aina 700 za samaki zimeorodheshwa katika beseni la mto, na imekadiriwa kuna jumla ya spishi 800- 900 za samaki. [3] Kati ya hizo ni nyingi ambazo ni muhimu katika biashara ya samaki wa kufuga nyumbani.

Marejeo

hariri
  1. Villa, Marco Aurelio. 1964: Aspectos geográficos del Territorio Federal Amazonas . Corporación Venezolana de Fomento. Caracas. 191p.
  2. Zinck, Alfred. 1986. Venezuelan rivers. Cuadernos Lagoven Lagoven, S.A. Caracas. 64p.
  3. Hales J. and P. Petry 2013. Rio Negro Ilihifadhiwa 1 Desemba 2017 kwenye Wayback Machine.. Freshwater ecoregions of the world. Retrieved 12 February 2013
  Makala hii kuhusu maeneo ya Brazil bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rio Negro (Amazon) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.