Saba ni kisiwa cha bahari ya Karibi (Amerika ya Kati). Kwa kiasi kikubwa kinaundwa na volkeno inayoweza bado kulipuka. Urefu wake ni mita 887.

Kisiwa cha Saba kutoka kaskazini: kilele cha Mount Scenery kimezungukwa na wingu.

Ni sehemu ya pekee ya Uholanzi.[1]

Eneo lake, pamoja na kisiwa kidogo cha jirani (Green Islet), ni kilometa mraba 13 tu.

Wakazi wa kudumu ni 1,991. Wengi wao ni machotara, ni Wakristo wa Kanisa Katoliki na huongea hasa Kiingereza, ingawa Kiholanzi ndicho lugha rasmi.

Makao makuu ni The Bottom.

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Saba (kisiwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.