Sabiniani wa Troyes

(Elekezwa kutoka Sabinianus wa Troyes)

Sabiniani wa Troyes (Samo, leo nchini Ugiriki, karne ya 3 - Rilly-Sainte-Syre, karibu na Troyes, Ufaransa, 275 hivi) alikuwa Mkristo aliyefia dini yake wakati wa dhuluma ya kaisari Aurelian[1].

Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 24 Januari[2].

Maisha

hariri

Alihama kisiwa alichozaliwa kwa sababu alivutiwa na Ukristo ila aliogopa upinzani wa baba yake.

Huko Galia alibatizwa na Patroklo wa Troyes.

Baada ya huyo kufia dini, Sabiniani aliendelea mwenyewe kuinjilisha na kubatiza hadi alipoteswa na kukatwa kichwa.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.