Saksonia-Anhalt (Kijerumani: Sachsen-Anhalt) ni moja ya majimbo 16 ya kujitawala ya Ujerumani lenye wakazi milioni 2,3 kwenye eneo la 20 446 km². Mji mkuu ni Magdeburg. Waziri mkuu ni Reiner Haseloff (CDU).

Mahali pa Saksonia-Anhalt katika Ujerumani
bendera ya Saksonia-Anhalt

Jiografia hariri

Saksonia-Anhalt imepakana na majimbo ya Ujerumani ya Mecklenburg-Pomerini, Brandenburg, Saksonia, Thuringia, Hesse na Saksonia ya chini.

Miji mikubwa ni pamoja na Magdeburg, Halle (Saale) na Dessau.

Elbe na Saale ni mito muhimu zaidi.

Kaskazini ya jimbo ni nchi tambarare; katikati kuna maeneo ya rutba kubwa katika mazingira ya Magdeburg. Kusini ni eneo la vilimavilima vinavyopanda juu hadi milima ya Harz.

Historia hariri

Jimbo la Saksonia Anhalt lilianzishwa mwaka 1945 kwa kuunganisha maeneo mawili: Mkoa wa Saksonia (Sachsen) wa Prussia na jimbo la Anhalt. 1949 likawa sehemu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (Ujerumani ya Mashariki). Kutokana na harakati ya kubadilisha utawala katika Ujerumai ya Mashariki jimbo liligawiwa kuwa mikoa 2 ya Halle und Magdeburg na jimbo lilifutwa.

Wakati wa maungano ya Ujerumani mikoa ya awali ilibatilishwa na jimbo la Sachsen-Anhalt liliundwa tena mwaka 1990.

Picha za Saksonia-Anhalt hariri

Tovuti za Nje hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Saksonia-Anhalt kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


 
Majimbo ya Ujerumani
 
Baden-WürttembergBavaria (Bayern)BerlinBrandenburgBremenHamburgHesse (Hessen)Mecklenburg-Pomerini Magharibi (Mecklenburg-Vorpommern)Saksonia Chini (Niedersachsen)Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen)Rhine-Palatino (Rheinland-Pfalz)Saar (Saarland)Saksonia (Sachsen)Saksonia-Anhalt (Sachsen-Anhalt)Schleswig-HolsteinThuringia (Thüringen)