Salami ni aina ya soseji yenye chumvi na viungo vingi isiyopikwa ikikaushwa hewani au katika moshi baridi[1].

Salami jinsi zinavyotengenezwa kwa wingi kiwandani.
Aina tatu za salami za Italia.

Asili yake iko katika nchi za Ulaya, jina limetoka katika Kiitalia kutoka Kilatini salare inayomaanisha kutia chumvi.

Salami inatengenezwa kwa kuchanganya nyama nyekundu na nyama ya mafuta baada ya kusaga yote mawili kwa vipande vidogo lakini ukubwa hutegemea aina yake[2].

Huko Italia zamani walitumia pia nyama ya punda na farasi kwa soseji hiyo lakini siku hizi mara nyingi ni nyama ya nguruwe. Kuna pia salami za nyama ya ng'ombe au nyama ya ndege kama bata mzinga au buni[3].

Kimapokeo nyama iliyosagwa na kutiwa chumvi na viungo hujazwa katika utumbo lakini siku hizi salami zinatengenezwa mara nyingi kiwandani ambako mirija ya plastiki hutumiwa.

Baada ya kujaza, aina nyingine hukaa tu hewani penye baridi ili zikauke na kuiva; aina nyingine huwekwa kwanza katika chumba chenye moshi baridi ambamo zinapokea ladha ya ziada halafu kukauka hewani.

Marejeo

hariri
  1. Salami Ilihifadhiwa 28 Agosti 2016 kwenye Wayback Machine., ufafanuzi katika kamusi ya Lexico
  2. Making salame at home, tovuti ya Italia
  3. Production of salami from ostrich meat with strains of Lactobacillus sake, Lactobacillus curvatus and Micrococcus sp, makala kwenye tovuti ya science-direct

Vungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Salami (chakula) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.