Soseji ni chakula kilichotengenezwa kwa nyama iliyosagwa au kukatwa kwa vipande vidogo, kuchanganywa na chumvi na viungo halafu kujazwa katika sehemu za utumbo au mirija ya plastiki. Kwa aina mbalimbali za soseji viwango vya nafaka au mkate vinaweza kuongezwa katika mchanganyiko.

Soseji zinazokaangwa
Kujaza soseji kwa mkono
Kutenganisha soseji

Jina soseji limeingia katika Kiswahili kutoka Kiingereza "sausage"; asili yake ni Kilatini "salsica" yenye maana ya "iliyotolewa chumvi".

Vipande virefu vinavyotokea baada ya kujaza hutenganishwa kwa kufunga sehemu kwa kamba au kuviringisha vipande vinavyoweza kukatwa baada ya kupika.

Soseji nyingi hupikwa baada ya kutengenezwa. Aina nyingine zinawekwa katika moshi juu ya moto zikiiva humo kwa muda wa siku au wiki kadhaa. Aina kadhaa hukauka tu hewani.

Soseji za kupikwa zinaweza kufungwa katika kopo au glasi ambako zinaweza kudumu muda mrefu.

Siku hizi soseji hutengenezwa mara nyingi kiwandani kwa kutumia mashine zinazosaga nyama nyingi na kutengeneza soseji mfululizo.

Soseji zimetengenezwa tangu kale. Kwa upande moja ni njia ya kutunza nyama kwa muda kabla ya matumizi kwa kuongeza chumvi inayoozuia bakteria na kuziweka katika moshi inayozuia wadudu kutega mayai mle. Mbinu hiyo ni vigumu katika mazingira ya joto pasipo jokofu.

Kwa upande mwingine soseji, hata kama zinaliwa mara moja, ni njia ya kutumia sehemu za nyama zisizopendeza peke yake, kwa mfano vipande vya kichwa, midomo, masikio, vipande vidogo vinavyopatikana kati ya mifupa, moyo, na viungo vya ndani ya mwili, pamoja na utumbo. Mara nyingi hata damu inaweza kutumiwa kwa aina kadhaa za soseji.

Soseji zinaweza kuliwa peke yake, pamoja na mkate baridi, zinaweza kupikwa pamoja na mboga ya majani.

Ziko aina zinazofaa kuliwa bila kupashwa moto.

Nchi nyingi na hata mikoa huwa na soseji za pekee ziazotautiana katika ladha na mwonekano.

Marejeo

hariri

Tovuti za Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Soseji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.