Sarah Wayne Callies

Sarah Wayne Callies (Sarah Anne Callies amezaliwa tar. 1 Juni 1977 huko La Grange Illinois) ni mwigizaji filamu na tamthiliya wa Kimarekani, anayejulikana vizuri baada ya kuigiza kama Dr. Sara Tancredi katika misimu miwili ya kwanza ya tamthilia ya Kimarekani Prison Break.

Sarah Wayne Callies

Sarah mnamo Januari 2015
Amezaliwa Sarah Anne Callies
1 Juni 1977 (1977-06-01) (umri 47)
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 2003 - hadi leo
Ndoa Josh Winterhalt

Wasifu

hariri

Miasha ya Awali

hariri

Callies na familia yake walihamia Honolulu, Hawaii. Kipindi hicho alikuwa na umri wa mwaka mmoja. Alianza kujionyesha mapema kuwa mapenzi yake ni kuigiza kwa kushiriki katika maigizo kadha wa kadha ya shuleni hapo Punahou School.

Wazazi wake wakiwa ni maprofesakatika chuo cha Hawaii kilichopo Manoa, Callies hakufuata nyayo zao kabisa. Badala yake, alichagua kujiingiza moja kwa moja kwenye Uigizaji. Alipohitimu elimu ya sekondari, alijiunga na chuo cha Dartmouth kilichopo Hanover, New Hampshire. Pamoja na kuwa na masomo, aliendelea kujihusisha kwenye maigizo.[1] Aliendeleza elimu yake hapo Denver's National Theatre Conservatory alipojipatia Shahada ya Sanaa ya Maigizo hapo 2002.[1]

Callies's alionekana mara ya kwanza kwenye luninga kama Kate O'Malley, uhusika wa mara kwa mara kwenye Queens Supreme. Aliigiza nafasi ya nyota kwa mara ya kwanza kama Jane Porter kwenye tamthiliya ya Tarzan, iliyorushwa na Warner Bros.

Baada ya kushirikishwa kwenye Law & Order. Special Victim Unit, Dragnet na NUMB3RS, Callies alikamata nafasi ya nyota kwenye Prison Break ya FOX kama Dr. Sara Tancredi. Pia aliigiza kama nyota kwenye filamu za Universal Picture za Whisper na The Celestine Prophecy.

Maisha Binafsi

hariri

Mnamo Juni 21, 2002, Callies alifunga ndoa na Josh Winterhalt, aliyekutana nae katika chuo cha Dartmouth. Winterhalt ni mwalimu wa sanaa. Ilipofika Januari 23, 2007, msemaje wake alitangaza kuwa wawili hao walikuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Julai 2007, Callies na mume wake walimkaribisha mtoto wao wa kike, Keala Winterhalt(Kay-AH-lah).[2][3]

Maigizo

hariri

Filamu

hariri
Mwaka Jina Kama
2006 The Celestine Prophecy Marjorie
2007 Whisper Roxanne
2011 Black Gold Kate Summers
Faces in the Crowd Francine

Tamthilia

hariri
Mwaka Jina Kama
2003 Queens Supreme Kate O'Malley
Law & Order: Special Victims Unit Jenny Rochester
Dragnet Kathryn Randall
Tarzan Jane Porter
2004 The Secret Service Laura Kelly
2005 NUMB3RS Kim Hall
2005 - 2007 Prison Break Sara Tancredi
2010 House M.D. Julia

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 Gary C.W. Chun (20 Machi 2006). "StarBulletin.com". Honolulu Star-Bulletin. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (Html) mnamo 2007-03-06. Iliwekwa mnamo 2008-03-05. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help); Text "/2006/03/20/" ignored (help); Text "Features" ignored (help); Unknown parameter |accessyear= ignored (|access-date= suggested) (help)
  2. Ausiello, Michael (23 Januari 2007). "Exclusive! Prison Break Leading Lady Pregnant! Ausiello Reports". TV Guide. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-04-01. Iliwekwa mnamo 2008-03-05. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help); Text "TVGuide.com" ignored (help); Unknown parameter |accessmonthday= ignored (help); Unknown parameter |accessyear= ignored (|access-date= suggested) (help)
  3. Nudd, Tim (23 Januari 2007). "Prison Break's Sarah Wayne Callies Is Pregnant - Pregnancy, Sarah Wayne Callies : People.com" (Html). People. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |accessmonthday= ignored (help); Unknown parameter |accessyear= ignored (|access-date= suggested) (help)

Viungo Vya Nje

hariri