Sebastiani mfiadini

(Elekezwa kutoka Sebastiano)

Sebastiani mfiadini (alifariki Roma, Italia, 288 hivi) alikuwa Mkristo aliyeuawa wakati wa dhuluma ya kaisari Diocletian dhidi ya imani hiyo.

Kifodini cha Mt. Sebastiani kilivyochorwa na Il Sodoma, 1525 hivi.

Mzaliwa wa Milano, Ambrosi anaeleza kwamba alifika Roma wakati dhuluma ilipokuwa kali akapatwa nayo akajishindia makao ya milele.

Tangu kale[1] anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Wa kwanza wanaadhimisha sikukuu yake tarehe 20 Januari[2], wa pili tarehe 18 Desemba.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. The details of Saint Sebastian's martyrdom were first spoken of by 4th-century bishop Ambrose of Milan (Saint Ambrose), in his sermon (number 22) on Psalm 118. Ambrose stated that Sebastian came from Milan and that he was already venerated there at that time.
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.