Senegalese kaftan

vazi la wanaume linalovaliwa Senegal

Senegalese kaftan, ni vazi la wanaume lenye mikono mirefu. Katika lugha ya Kiwolofu, vazi hili huitwa mbubb au xaftaan na kwa lugha ya Kifaransa huitwa boubou .

Kaftans mbili za Senegal zikivaliwa nchini Cameroon, kulia.

Caftan ya Senegal ni vazi lenye urefu sawa na kifundo cha mguu. Huvaliwa na suruali yenye kamba iitwayo tubay kwa Kiwolof . Kwa kawaida hutengenezwa kwa pamba, lazi, au vitambaa vya sintetiki, majoho haya ni huvaliwa kote Afrika Magharibi . Kaftan na suruali zinaofanana huitwa suti ya kaftan . [1] Suti ya kaftan inaweza kuvaliwa na kofia ya kufi . Kaftans ni mavazi ambayo huvaliwa katika nchi zote za Afrika Magharibi. Nchini Marekani, baadhi ya wafanyabiashara huuza vazi hili kama seti ya suruali ya dashiki ya mtindo wa Senegali. Wanaume ambao ni watu wa kabila la Hausa, huvaa kaftan hizi kwenye hafla mbali mbali kama vile sherehe za harusi. Nchini Marekani, kaftan ni mojawapo ya suti tatu rasmi, sawa na tuxedo, ambazo wachumba wa Afrika na Amerika huchagua kwa ajili ya harusi zao. Mitindo mingine ikiwa ni paoja na seti ya suruali za dashiki, na grand boubou, pia hutamkwa gran boo-boo.  

Marejeo hariri

  1. "Be a Power Dresser this Year". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-06. Iliwekwa mnamo 2022-03-17.