Sereno wa Marseille

Sereno wa Marseille (karne ya 6 - Vercelli, Italia, 601 hivi) alikuwa askofu wa 10 wa Marseille, katika Ufaransa wa leo, kuanzia mwaka 596 hivi hadi kifo chake[1].

Mt. Sereno alivyochorwa.

Papa Gregori I alimuandikia barua nne zilizotufikia[2][3].

Alipokea kwa ukarimu Augustino wa Canterbury na wenzake waliotumwa na Papa huyo kuinjilisha Uingereza[4].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Agosti[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.