Shikamoo ni neno lenye asili ya Kiarabu linalotumiwa kumsabahi mtu. Maana ya neno hilo huelezwa kuwa kifupi cha "nashika mguu wako" kama tamko la heshima mbele ya mkubwa. Hivyo ni salamu inayotumiwa na wadogo kwa wale wanaowazidi umri, hasa wazee. La sivyo, salamu kama "habari za sasa hivi" hutumika.

Jibu lake ni "Marahaba", salamu inayotumiwa kati ya Waarabu sawa na "hujambo", ila kwa matamshi ya "marhaba". Pale jibu ni "marhabteen" yaani marhaba mara mbili.

Matumizi yake ni kawaida katika Kiswahili nchini Tanzania, kumbe huko Kenya mara nyingi haieleweki isipokuwa kwenye maeneo ya pwani.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shikamoo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.