Sidoni

(Elekezwa kutoka Sidon)

Sidoni (kwa Kiarabu صيد, Ṣaydā, kwa Kigiriki Σιδών, Sidon) ni mji wa Lebanoni kusini, katikati ya Beirut na Tiro, maarufu katika historia ya kale hasa kwa utajiri uliotokana na biashara yake ya kupitia baharini. Hata leo unategemea sana bandari yake, mbali ya utalii.

Sidoni leo.
Ngome iliyojengwa na askari Wakristo wa Vita vya msalaba mwaka 1228.
Ndani ya Old Souks.
Ngome ya Mt. Luis.
Ndani ya Khan El Franj.
Kisiwa cha Ziri.

Wakazi walikuwa 65,000 hivi mwaka 2000, lakini pamoja na eneo la kandokando wanafikia 200,000[1][2] na kuufanya mji wa tatu nchini Lebanoni.

Katika Biblia

hariri

Katika Biblia mji huo unatajwa mara nyingi, kuanzia Kitabu cha Mwanzo hadi Injili na Matendo ya Mitume.

Wengi kutoka maeneo yake walikwenda kumsikiliza Yesu (Mk 3:8; Lk 6:17), naye alitembelea maeneo yake (Mk 7:24; Math 15:21) na kusema ungetubu mapema kuliko Wayahudi wenzake aliowahubiria kwa kuwapa uthibitisho wa miujiza mingi (Math 11:21-23).

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sidoni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.