Silvano wa Homs (alifariki Homs, Syria, 311 hivi) alikuwa kwa miaka arubaini askofu wa mji huo ambaye aliuawa kwa imani ya Kikristo kwa kutupwa pamoja na shemasi Luka na msomaji Mosyo waliwe na wanyama wakati wa dhuluma ya kaisari Maximinus[1].

Mchoro mdogo wa kifodini chake na cha wenzake Luka na Mosyo.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Februari[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.