Sipriani wa Unizibira

Sipriani wa Unizibira (alifariki 482) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji wa Unizibira (leo Henchir-Zembra kusini mwa Tunisia).

Alifariki pamoja na askofu Felisi wa Abbir kutokana na dhuluma ya Huneriki, mfalme wa Wavandali, ambaye alikuwa mfuasi wa Ario na alihamisha Wakatoliki 4,966 (au 4,976) wakaishi katika jangwa la Sahara kwa lengo la kuwafanya wafe kwa njaa. Baadhi waliuawa na askari njiani[1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 12 Oktoba[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.